
Bustani ya wanyama ya Nashville Tennessee Marekani, imesheheni wanyama wengi waliosafirishwa toka sehemu mbalimbali za Afrika ikiwa ni pamoja na mbuga maarufu ya Serengeti. Si wanyama tu, ukiangalia kwenye hiyo picha hapo juu utaona kuna mfano wa ngao ya kimasai. Hawa jamaa wameeleza moja kwa moja kuwa asili ya ngao hiyo ni Tanzania kwenye kabila la wamasai.
Pia kuna picha mbali mbaali za mabinti wa Kimasai zianonekana kwenye mbao za matangazo kwenye hiyo bustani. Ninalojiuliza ni kwamba picha hizo zilippigwa kihalali? Je hao mabinti au wazazi/walezi wao walitoa idhini? Je walilipwa haki yao? Je walijua picha zao zitakuwa kwenye mbao za matangazo zikiingiza fedha kwa kila mtu anayeingia kwenye bustani hiyo?
TAmaduni zetu zinazotoweka taratibu kwa wenzetu zimebakia kuwa chanzo kikubwa cha mapato.
No comments:
Post a Comment