
Mila na desturi ni dhana zinazomtambulisha mtu awapo pamoja na watu wengine. Ni muhimu kuziheshimu na kuzienzi, hata hivyo wakati inapobidi, baadhi ya mila inapasa zichunguzwe na kuwerekebishwa hasa pale mila hizo zinapoleta madhara kwa jamii moja kwa moja au kwa kupitia kwa viumbe vingine. Tunapozizungumza mila hizi hasa kwa watu wasiozifahamu, hatuna budi kuwa maini sana ili kuepuka kudharaulisha nchi yetu kwa wageni wasioifahamu.
Japo twappaswa kuzipiga vita mila zenye madhara, inatupasa kuwa makini hasa tunaposema tukiwa nje ya Tanzania. Watu wa nchi za magharibi, wamekuwa na mtazamo hasi sana juu ya bara la Afrika, hivyo kudharau mila na desturi za waafrika pasipokujua mila hizo ni kiungo kikubwa kwa jamii za waafrika na kwamba kwa namna moja au nyingine zina umuhimu wake katika jamii.
Mwezi wa kumi na moja mwaka jana 2006, nilipata nafasi ya kuwasilisha mada ya Ukeketaji kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu. Nilipokea maswali mengi ikiwa ni pamoja na kuhusu uchaguzi wangu wa kutumia neno FEMALE CIRCUMCISION na si MUTILATION. Maneno haya yote ambayo yanalenga jambo moja ya TOHARA KWA WANAWAKE au UKEKETAJI, yanatumiwa yakiwa na maana zilizozidiana uzito.
Mimi kama mtu ninayeipenda nchi yangu, utamaduni wangu na kuuheshimu, nilipata wakati mgumu kutafuta namna ambayo ningezungumzia suala hili la UKEKETAJI bila kuwatukana wazee waliodumu na mila hii japo si nzuri.
Wazo langu la msingi hapa ni kwamba japo mila fulani zimeonekana kuwa na madhara kwa binadamu, tunapozizungumza tunapaswa kuwa makini sana tukijaribu kwa kila njia kuepuka kudhalilisha au kutukana utamaduni wa nchi yetu na asili yetu kwa ujumla. Ni muhimu kupiga vita mila potofu, lakini namna tunavyolijadili suala zima, ina madhara au manufaa makubwa sana kwa uelewa wa watu kuhusu nchi yetu. KUMBUKA MDHARAU VYA KWAO NI MTUMWA.
2 comments:
Taratibu mila zenye mapungufu zitapotea!
Ni kweli kabisa na inapasa tuzipige vita lakini kwa akili
Post a Comment