Friday, September 28, 2007

Kumbukumbu za Maisha

Maisha ni safari ndefu, yanatupitisha katika nyakati fulani ambazo hazisahauliki kamwe maishani. Usiku huu pale chini ya Mdigrii mti maarufu pale chuo kikuu cha Dar es salaa, vichwa vilikuwa vikiumia juu ya swali la Isimu lililoulizwa darasani na majibu yake yakawa tabu kidogo kupatikana. Kumbuka tupo 60 Darasani na vitabu ni viwili tu maktabani. Hata hivyo staili hii ya usomaji ilikuwa inatutoa kwani kila mtu alichangia kidogo alichoelewa hatimaye kitu kizima kilipatikana. Kwa bahati mbaya sana mmoja kati ya waliopo hapo ni marehemu sasa, loh!! Inasikitisha sana kwani darasa lote tuliishi kama ndugu, anapotoweka mmoja ghafula ni maumivu makubwa moyoni

1 comment:

MTANZANIA. said...

Tulimpenda Matemu, Lakini Mola kampenda zaidi. Tumuombee kwa Mungu apumzike kwa Amani.

Bye.