Tuesday, January 22, 2008

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo!!!

Mtoto anayeonekana pichani, nilimkuta akiwa na baba yake juu ya ziwa monona ambalo limeganda sasa kutokana nabaridi kali iliyotawala maeneo mengi ya Marekani. Hapo alipo ameanguka baada ya kuteleza kwenye theluji. Kina cha maji kwenye eneo alilopo huyo mtoto lina pata mita kama kumi hivi. Lakini kutokana na hali ya kuganda, ni salama tu kutembea hapo juu. Wasiwasi wangu ni hiyo baridi na huyo ni mtoto mdogo. Kumbe ndio maana wengi wa wamarekani hawapati shida sana kipindi cha baridi kama inavyotokea kwa wabongo. Wamekuzwa wakiizoea baridi. Ama kweli mtoto umleavyo ndivyo akuavyo

1 comment:

Anonymous said...

Hello. This post is likeable, and your blog is very interesting, congratulations :-). I will add in my blogroll =). If possible gives a last there on my blog, it is about the Celular, I hope you enjoy. The address is http://telefone-celular-brasil.blogspot.com. A hug.