Pichani ni Mnyororo na tufe lenye uzito wa zaidi ya Kilo 30 lililogunduliwa hivi karibuni na Dk. Fred Nyanda hapa Tennessee Marekani. Inasemekana Mnyoror0 na tufe hili vilitumika kuwafungia watumwa wasitoroke kipidi cha biashara ya utumwa. Ni jambo lisiloelezeka jinsi ambavyo binadamu anaweza kumfanyia binadamu mwenzie unyama wa namna hii. Mzungu anayemiliki nyumba ulipogunduliwa mnyororo huo alijisikia aibu wakati mzee Nyanda alipokuwa anauchukua mnyororo huo. Ugunduzi wa mambo haya unatonesha makovu yaliyosababishwa na historia nzima ya Ukoloni na utumwa.
Mengi zaidi kuhusu mnyororo huu yapo jikoni yanakuja
Mengi zaidi kuhusu mnyororo huu yapo jikoni yanakuja
2 comments:
Ticha!
Nimependa staili ya blogu yako, natumai wadau wengine wanaipenda pia. Nitaitembelea kila siku!
Nimepitia hapa na hii habari inanikumbusha ukiwa.Sasa huyo mzungu alikuwa anauhifadhi huo mnyororo ili autumie tena kwa shughuli ile2 au? Nitafuatilia maelezo.
Post a Comment