Chama cha watanzania waishio jimbo la Tennessee Marekani (MTTA)kimejipatia uongozi mpya baada ya uongozi wa zamani kumaliza muda wake. Toka kulia ni Dk. Mkoma ambaye ni makamu mwenyekiti, Bi. Esther Idassi - Katibu, Bw. September Nyang'oro- Mwenyekiti, Dk. Margret Mbaga, mtunza hazina, na Bi. Winnie Mushi MBye ni katibu anayestaafu. Katika kipindi cha uongozi uliopita chama kilifanikiwa kupata usajili, na kilizinduliwa rasmi na mheshimiwa balozi Andrew Mhando Daraja, aliyekuwa balozi wa Tanzania hapa Marekani. Tunawapongeza viongozi waliomaliza muda wao kwa kazi nzuri, na tunawakaribisha viongozi wapya.
No comments:
Post a Comment