Tuesday, January 16, 2007

OPRAH

Oprah ajenga shule ya kifahari ya Wasichana Afrika Kusini

Bila shaka mmesikia habari ya Oprah Winfrey kufungua shule ya wasichana huko Afrika Kusini. Shule enyewe inaitwa ‘The Oprah Winfrey Leadership Academy’. Kwa kweli nampongeza kwa kitendo chake cha kukumbuka Afrika na kusaidia wasichana huko. Wanafunzi waliochaguliwa wanatoka kwenye familia zenye kipato cha chini. Na walichaguliwa kutoka kwa maelfu ya wasichana walioomba nafasi ya kuingia huko.Oprah alijenga shule hiyo kwa gharama ya dola za kimarekani $40 milioni. Kwa sasa ina wanafunzi 145. Bila shaka tutasikia waliosoma hapo watapata mafanikio mazuri kimasomo na kwenda kusoma vyuo vikuu maarufu duniani kama Harvard, Stanford, Cambridge, Oxford etc.Shule enyewe ni ya kifahari hasa. Hata wanaosoma shule za Ivy League na ma Prep school duniani wanaweza kuwaonea wivu hawa wasichana. Nikisema ni ya kifahari, nina maana ni ya kifahari hasa. Oprah mwenyewe ni bilionea na kazoea maisha ya kifahari na alitaka hao wasichana wajue ufahari manake nini. Mfano, shule ina saluni kwa ajili ya kutengeneza wasichana nywele, wanalalia mashuka yenye nyuzi 200 count (Duh…kama wanalala hoteli ya Waldorf Astoria) sahani zilichaguliwa na Oprah na si ajabu sahani moja ina gharama ya dola mia, ina theatre za ndani na nje, ina ma fireplace tele (Afrika unahitaji fireplace ya nini?) na mengine mengi. Walimu wameletwa kutoka nchi za nje.Je, wakirudi majumbani mwao kwa ajili ya likizo wataishi namna gani? Si wamezoea ufahari. Si uwongo kuna watu ambao baada ya kukosa maisha ya kifahari waliozoea, walirukwa na akili na wengine kujiua kalcha shoku. Natumaini Oprah ana mpango wa kuhakikiisha hao wasichana wanaendelea kuishi maisha ya kifahari wakimaliza masomo yao.
Vipi nyie mwaonaje?

5 comments:

MTANZANIA. said...

"Ama kweli mcheza kwao hutuzwa","vilevile damu ni nzito".Pamoja na utajiri alionao lakini bado anakumbuka kuisaidia jamii yake ya asili.Kwa wale msiokuwa na taarifa ni kwamba Oprah asili yake ni jimbo la Kwazul-Natal nchini Afrika.Huko ndiko walikotoka wazazi wake kabla ya kuhamia nchini Marekani.Urithi pekee kwa watoto ni elimu. "Wakatabahu"

Anonymous said...

Ndio mana watu wengine utajiri wao unaongezeka kila mara. Hivi unadhani kwa nini mtu kama huyu Munu asimfungulie mibaraka ya aambinguni! Atoaye kwa moyo hurejeshwa kwa kiwango kile kile au mara dufu

Anonymous said...

Mimi nilisikia kuwa Bi Oprah alitoka kwenye familia yenye kipato kidogo sana,hivyo nafikiri tofauti na wale waliotoka ktk hali kama hiyo yeye ametaka hao wasichana ktk shule yake waanze kuelewe umuhimu wa elimu ya kitajiri,kazi nzuri na ya uhakika baada ya elimu hiyo.Anajua kuwa utajiri wake si kitu kama mamilioni ya weusi wenzie hasa wasichana hawatasaidiwa na yeye na wengine wenye utajiri kama yeye kuondokana na umaskini walio nao.Ktk mazingira haya watachukua mfano mzuri kutoka kwa Bi Oprah na washirika wake.Sisi weusi huwa tunasahau kuwa umaskini wa wengi wetu unatuhusu wote.May God bless you Bi Oprah!!

Anonymous said...

http://restaurants-us.com/oh/Cincinnati/Bonefish%20Grill%20-%20Hyde%20Park/45209/

Anonymous said...

Directory of insurance agencies organized by states http://insuranceinstates.com/florida/Tampa/Transamerica%20Long%20Term%20Care/33637/