Monday, April 30, 2007

MLO WA KITANZANIA HASWA



Mapochopocho kadha wa kadha yalikuwepo, ilimradi kila mtu alifurahia. Huku baadhi ya mboga za majani zinaliwa bila kupikwa kama inavyoonekana hapo juu. Jamaa mmoja ambaye hakuwa amezoea huu mlo wa namna hii yalimkuta ya kumkuta siku moja. Jamaa alifika Marekani akiwa hana mwenyeji wa kueleweka, hivyo baadhi ya mambo mengi ya kitamaduni ilibidi ajifunze tu mwenyewe. Siku moja mchana jamaa akiwa kachoka kweli, akaingia mgahawani. Kama ilivyo kawaida ya wageni wengi wanaoingia Marekani kwa mara ya kwanza na ambao hawakuwa na mazoea ya kuingia ingia migahawani kule nyumbani, ilimwia jamaa vigumu kidogo kuelewa kilichoandikwa kwenye Menyu. Mhudumu nae alikuwa mmarekani mweusi na alikuwa anaongea kwa haraka kidogo hivyo ikawa vigumu kidogo kwa jamaa kuelewa aagize nini. Hivyo kwa kutizama picha jamaa akachagua chakula kimoja kilichoonekana kama kina nyama nyingi nyingi hivi. Baada ya muda, binti mhudumu alirudi akiwa na kinywaji, jamaa alikipokea na kuanza kubugia, mara kidogo binti karejea tena na sahani imejaa mchicha lakini mbichi, jamaa alitamani alie kwani alijua ndio chakula kimekamilika hivyo.

2 comments:

MTANZANIA. said...

Duh! Mambo ya mnuso. Lakini huku ni kutamanishana bwana Mgonja.

Ila hata mimi mhhhhh! Kula majani mabichi ka mbuzi hapana. Najua yana virutubisho ila si haya ya kutoka US. Haya yana viathirishi badala ya virutubisho. Na hii ni kutokana na namna yanavyokuzwa kitaaluma.

Blog yako inaita. Teh teh!

Zablon Mgonja said...

Asenti