Monday, January 15, 2007

Mwalimu Abou Salimu, aliyesimama kulia mwenye koti jeusi, Mbongo mwingine anayekuja kasi katika fani ya ufundishaji wa Kiswahili huku Marekani. Hapa yupo na wanafunzi wake huko Chuo kikuu cha New York Marekani. Mwalimu Abou anasifika sana chuoni New York kwa uwezo wake wa kutumia zana za kisasa za kufundishia kama vile Multi media smart cart na kadhalika. Wanafunzi wake pia wamemsifu kwa umahiri wake wa kulandanisha lugha na utamaduni wa watu wa lugha hiyo. Laiti serikali yetu ingetambua umuhimu wa waalimu kama wanavyotambuliwa katika nchi nyingine, waalimu wangefundisha kwa moyo na kiwango chetu cha elimu kingekuwa juu sana.
Hata hivyo, waalimu mliopo mbali na nchi yenu, tambueni kuwa Tanzania bado inawahitaji sana, Tanzania ya kweli itajengwa na wataalamu kama nyie. Hivyo pamoja na kuwafunza waghaibu, kumbukeni HOME IS ALWAYA THE BEST. Asante kwa juhudi zako mwalimu endelea kukomaa,... Kwa wengine mnaofanya mambo kama haya tafadhali nitumieni picha na maelezo ili tujadili


1 comment:

Anonymous said...

Ina maana kiswahili ni kwa ajili ya weusi tu? Mbona wazungu siwaoni?