Sunday, January 14, 2007

Mwalimu Method Mechardes Rutechura ( Katikati mwenye Tshirt nyeupe na Jeans ya bluu) Kijana aliyejizolea umaarufu hapa Marekani kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukimiliki Kiswahili awapo mbele ya Darasa. Hapa anaonekana akiwa na wanafunzi wake Katika chuo kikuu cha SIT kilichopo Brattleboro,Vermont Marekani. Kwa sasa mwalimu Rutechura anakingurumisha Kiswahili katika Chuo kikuu cha Madison Winsconsin MArekani. Nchi yetu inahitaji vijana kama hawa wenye vipaji na taaluma waliopikwa wakaiva katika fani. Mambo haya yakiendelea namna hii, Tanzania yetu itazidi kuwa maarufu na hili litacochea maendeleo yetu yanayochechemea. Tunawahitaji vijana kama hawa kuondoa Giza lililosheheni kwenye vichwa vya watu wengi wa nchi za magharibi kuhusu bara la Afrika. Wengi hudhani kuwa Afrika ni nchi moja tu kuuuubwa na kwamba watu wake wote wanajuana.
Hongera Professa- Kama wanavyokuita wanfunzi wako huku, kaza kamba safari bado ndefu

3 comments:

MTANZANIA. said...

Inafurahisha kusikia kiswahili chetu kinafundishwa nchi zanje.Bwana Mgonja unaweza kunifahamisha nafasi ya kiswahili miongoni mwa lugha kuu duniani?

Anonymous said...

Kumbe nabii haheshimiki nyumbani!!
Hawa vijana walioko Marekani wakiitangaza Tanzania, wakirudi nyumbani wala serikali haiwezi kuwafikiri.Kweli Mwl. Nyerere alisema:"Tanzania itajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno".
Hongera "Mbabe wa Kivita" kaza moyo katika kukitangaza Kiswahili ughahibuni.

Anonymous said...

Aminia kaka.endelea kuinkopareti lugha na utamaduni. Ni muhimu sana kaka.